Menu
 

Msanii Ney Lee akiwa location.

The Super Woman kama anavyojiita mwenyewe NEEMA AGREY a.k.a NEY LEE  ambaye ni hitmaker wa Umekwenda amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuchelewa kuiachia filamu yake SUPER WOMAN iliyotakiwa kutoka mapema mwaka huu na kwamba soon ataiachia baada ya kumalizia scene ya mwisho jijini Mbeya.


Akichanika kupitia Bomba Base Show ya Redio Bomba FM mwimbaji NEY LEE alikuwa na maneno haya ya kuwaridhisha mashabiki wake ''Filamu ipo tayari karibia namalizia kushoot, lakini samahani kwa watu wangu kwa kuchelewa kuiachia kutokana na sababu zilizokuwa juu ya uwezo wangu kwa hiyo nitatangaza ni lini nitaiachia ambapo natarajia uzinduzi wa filamu yangu ya SUPER WOMAN nitazindua na Kitabu changu cha Super woman na video ya Kinyonga niliyomshirikisha Linnah, na Madee''.


''Katika filamu yangu nimewashirikisha Ma-Star wengi wa bongo hivyo nimeamua kutowaweka wazi itakuwa kama surprise, lakini location kubwa imetawala maeneo mengi ya Dar es salaam lakini pia mikoa ya jirani kama Iringa lakini natarajia kurudi na huko nyumbani kucha kumalizia kipengele huko ili kuitangaza Mbeya yangu/yetu katika anga za kimataifa na baadhi ya Ma-Star wa huko nyumbani pia watapata fursa ya kushiriki katika filamu''. alimalizia kwa kusema hivyo NEY LEE.

Post a Comment

 
Top