Menu
 

Liverpool wamefikia makubaliano ya kumuuza Luis Suarez kwenda Barcelona. Ada ya uhamisho inadhaniwa kuwa takriban pauni milioni 75.

Suarez alijiunga na Liverpool mwaka 2011 akitokea Ajax, kwa pauni milioni 22.7. Alikuwa amesalia na miaka minne katika mkataba wake uliokuwepo na Liverpool. 

Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa England, baada ya kupachika mabao 31 ya ligi msimu uliopita.

Suarez kwa sasa anatumikia adhabu ya miezi minne na mechi tisa za kimataifa kwa kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italy wakati wa mechi ya Kombe la Dunia Brazil.

 
Kupata uhondo wakutembelea Bofya Hapa

Post a Comment

 
Top