Menu
 


Mwalimu Laiton Jackson Ngoli(46)wa shule ya awali Kijiji cha Maendeleo Ishungu Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufundisha watoto zaidi 300.

Shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi  wachache yenye madarasa mawili yasiyo na vipimo sahihi hayana madawati hivyo kuwafanya wanafunzi kusoma katika mazingira magumu.


 
Hata hivyo juhudi binafsi za Mwalimu Ngoli asiye na taaluma ya ualimu bali kufanya kazi hiyo kwa uzoefu baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari Malangali mwaka 1994 na kufungua shule hiyo ambayo haina usajili miaka saba iliyopita.


Shule hiyo ilifunguliwa na wakazi wa Ishungu kutoka shule ya msingi ya Ruiwa ili watoto waweze kusoma kutokana na kujaa kwa maji wakati wa mvua za masika ambazo husababisha mto Gwili kujaa maji na kuwafanya watoto kushindwa kuhudhuria masomo.


Aidha Mwalimu huyo amekuwa katika wakati mgumu kutokana na kufundisha watoto bila kulipwa takribani miaka saba tangu kufunguliwa licha ya wazazi kutakiwa kuchangia shilingi elfu moja kila mwezi lakini wazai wameshindwa kumudu kumlipa.Kwa upande wake Mweyekiti wa Kijiji cha Maendeleo Charles Galus Mkisi amekiri kuwepo kwa tatizo la kusajiliwa kwa shule hiyo ingawa wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kutoka ngazi ya Kijiji ,Kata na Wilaya bila mafanikio ingawa uongozi wa ngazi hizo umekuwa ukifika kutoa ushauri.


Baadhi ya wazazi wenye watoto shuleni hapo aliwemo Kuzenza Mtogwambuli na Jackson Halinga wameiomba Serikali kuisajili shule yao ili kuepusha utoro kwa watoto ambao hulazimika kutembea umbali wa kilometa nane ili watoto wa darasa la nne na la saba kuwasaidia kufanya mtihani wa Taifa.

Changamoto nyingine katika kijiji hicho ni ukosefu wa vyoo licha ya idadi kubwa ya watoto wengi ina matundu matatu ya vyoo ambavyo pia havija ezekwa.


Mtendaji wa Kijiji Mashaka Daud alisema wanapanga utaratibu wa kuunda kamati ya kukusanya pesa kwa ajili ya kulipa mwalimu aliyeamua kufundisha kwa kujitolea kwa miaka saba bila mshahara wowote.

Aidha, Serikali kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) Katika sekta ya elimu imetaja baadhi ya mipango itakayotumia kumaliza tatizo la watoto wasiojua kusoma na kuandika katika shule za msingi na sekondari nchini.

 Akizungumza katika mahojiano maalumu na kituo hiki Meneja Idara ya mawasiliano BRN, Anastazia Rugaba ametaja baadhi ya mipango hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo elekezi kwa walimu, kutoa motisha kwa wanaofanya vizuri na kulipa malimbizo ya fedha wanazodai.

Sambamba na hayo ni pamoja na kuanza kupeleka fedha za ruzuko moja kwa moja katika miradi ya shule husika badala ya kupitia katika serikali Za mitaa kama ilivyokuwa inafanya.

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) inasema watu wasiojua kusoma na kuandika Duniani wamefikia 774 milioni .

Kwa upande wa Tanzania hadi kufikia mwaka 2002 idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa watu 6.2 milioni. Idadi hiyo ni kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ambao ni sawa na asilimia 31, lakini kwa sasa idadi hiyo inaelezwa kuongezeka na kufikia watu zaidi ya milioni 14.

Ripoti hiyo inaeleza wazi kuwa idadi kubwa ya watu hao wasiojua kusoma na kuandika wengi wao wanaishi katika bara ya Afrika na Asia, na kwamba takwimu hizo zinaonyesha kiwango hicho kimeongezeka wa asilimia nane kuanzia mwaka 1990.

Kwa picha za tukio Bofya Hapa

Post a Comment

 
Top