Menu
 


Klabu ya mpira wa Miguu ya Real Madrid yenye maskani yake nchini Uhispania imeongoza katika orodha ya Forbes ya timu zenye thamani zaidi duniani.


Real Madrid, walioshinda Champions League mwezi Mei, ina thamani ya takriban dola Bilioni 3.44, kwa mujibu wa Forbes, ambayo imetaja klabu nyingine tatu bora zote ni timu za soka. 


Barcelona FC imeshika nafasi ya pili, ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.2 na Manchester United ni ya tatu ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.81.

Forbes imetathmini thamani ya timu hizo kwa kutazama thamani ya hisa, madeni na mikataba ya viwanja vyao.


Timu ya New York Yankees ya baseball ya Marekani imeshika nafasi ya nne ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.5. Nafasi ya tano inashikiliwa na Dallas Cowboys ya mchezo wa American Football ambayo ina thamani ya dola bilioni 2.3.  Pata uhondo zaidi kwa kutembelea Bofya Hapa
 
Top