Menu
 


*Angel Di Maria kwenda Man U
*Schneiderlin kwenda Arsenal
*Cech kuodoka Chelsea

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 80 kwenda Barcelona katika saa 48 zijazo (Daily Mail), dau la Liverpool la pauni milioni 20 la kumtaka beki Dejan Lovren limekataliwa na Southampton (Liverpool Echo), 

Manchester United wamepewa Angel Di Maria na Real Madrid kwa pauni milioni 40.  Arsenal, Paris St-Germain na Juventus pia wanamtaka pia mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina (Daily Star).

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika wa kuwasajili Alexis Sanchez na Mathieu Debuchy kwa pauni milioni 35 (Daily Mirror), washika bunduki hao pia watatoa dau la pauni milioni 20 kwa Southampton kumsajili Morgan Schneiderlin, ambaye anasakwa pia na Napoli (Daily Express), Bayern Munich huenda wakawazidi kete Manchester United, Liverpool na Arsenal kumchukua winga wa Fiorentina, Juan Cuadrado (Daily Express).

 Arsenal pia wametoa dau la pauni milioni 23.8 kumwania kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira na watamtumia rafiki wake wa karibu Mesut Ozil kumshawishi (Metro).

Dau la pauni milioni 32 la Manchester City kumtaka beki Eliaquim Mangala limekubaliwa na Porto, lakini bado wanasubiri kama Chelsea nao pia watapanda dau (Daily Star).

 Juventus wako makini kumsajili beki wa Manchester United Patrice Evra, ambaye amesaini mkataba mpya Old Trafford mwezi uliopita (Talksport).

 Barcelona wataajiri mwanasaikolojia wa kumsaidia Luis Suarez kukabiliana na 'mizimu' atakapokamilisha uhamisho wake (Sun).

QPR wanatarajia kukamilisha usajili wa Rio Ferdinand wiki ijayo (GetWestLondon), na kipa wa Chelsea Petr Cech huenda akaondoka Darajani kabla ya msimu mpya kuanza, kwa mujibu wa wakala wake (Talksport).

Post a Comment

 
Top