
Aliyekuwa mke wa Afande Sele (Waliachana baadae) aliyezaa
nae watoto wawili (Tunda na Sanaa) amefariki majira ya sita usiku wa
kumkia leo.
Akiongea na tovuti ya Times Fm kupitia simu ya Afande Sele, msimamizi
wa kazi za Afande Sele aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Busanda
amesema kuwa mama Tunda alifariki kutokana na ugonjwa wa malaria
uliomsumbua kwa muda wa siku tatu.
“Alilazwa katika hospitali ya St. Mary Morogoro akatolewa jana lakini
usiku hali yake kidogo ilizidiwa akapelekwa hospitali kubwa ya Morogoro
na umauti ukamkuta hapo. Aliugukua kwa muda wa kama siku tatu.” Jackson
Busanda ameiambia tovuti ya Times Fm.
Akizungumzia hali ya Afande Sele kwa sasa, amesema kuwa Afande Sele alizimia baada alipokuwa anaenda kuuona mwili wa marehemu.
Kuhusu utaratibu wa mazishi, amesema kuwa familia imepanga kufanya
mazishi leo majira ya saa tisa mchana katika makabuli ya Kola, mjini
Morogoro.
Marehemu ameacha watoto wawili ambao ni Tunda na Sanaa.
Tunampa pole Afande Sele, tunamuombea apate nguvu ya kuvuka kipindi hiki kigumu.
Mama Tunda apumzike kwa amani. Amina.
Afande aliandika ujumbe kwenye Facebook na Instagram kutoa taarifa ya msiba huo.