Menu
 

  

Masaa machache yamesalia ya uzinduzi wa Rise & Shine Mixtape ni kanda mseto ya Mwanamuziki LIL STIGGAR inayosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya Watanzania, ambayo imebebwa na vionjo mbalimbali vyenye kukonga nyoyo za mashabiki lukuki.

  Dhahiri shairi muziki unadaiwa kuwa ni moja ya tiba kwa wangonjwa baada ya watafiti kadhaa nchini Marekani kuwaweka wagonjwa 100 katika chumba chenye muziki na wengine 100 kupelekwa hospitalini lakini waliowekwa katika chumba maalumu chenywe muziki walioneka kupona mapema, kwa mantiki hii basi Kanda mseto ya RISE & SHINE ya LIL STIGGAR ni dozi tosha.

  Mwanamuziki LIL STIGGAR ni msanii anayetokea Kundi la umoja wa wasanii wa kike nchini Tanzania liitwalo FeMCTZ na wasanii wengine wanaounda kundi hilo ni pamoja na Cindy Rulz, Stosh, Tamy, Tiffer, Nat E na kiongozi wao Chiku K. 

PATA UHONDO KIDOGO KUTOKA KWA LIL STIGGAR


  Kanda Mseto ya RISE & SHINE itabeba jumla ya nyimbo 7 na Bonus Tracks, Shows mbalimbali alizozifanya LIL STIGGAR, Video za ngoma/nyimbo zake pamoja, lyrics pamoja na Biography ya msanii huyo LIL STIGGAR, ambavyo vyote kwa pamoja vitakuwa katika mfumo wa DVD.

  Wasanii walioshirikishwa katika Kanda Mseto hiyo ni pamoja na Phyno, Ammy Chiba, Gest Lydar, Chris Daniel, Ottuck, Zax B, Sauti from East na Anno Melody, na Maprodyuza waliohusika kuitengeneza Rise & Shine Mixtape ni Phyno Touchz, Dayo Music, Mg Creator, Losso Touchz, Gachi, Nachi & Waisa, Kingson na Kebby.

  Uzinduzi wa RISE & SHINE MIXTAPE unafanyika leo Agosti 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Mtenda Sunset Conference kwa kiingilio cha Shilingi 10,000/= ambapo Tiketi zimeanza kuunzwa mapema kuanzia sasa wahi mapema kununua tiketi kupitia simu ifuatayo 0654 079 930. Uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii kibao huku Red Carpet, Dancing na Maonesho ya mavazi ya Kiafrika yaliyopewa jina la "SONDELA".

  Uzinduzi huu umedhaniwa na Bomba FM Radio, Mbeya FM, The Premier Show ya G FM, Life Partners ENT, Sweet FM, Highlands FM, T Motion Films, Elishadai Records, Chimbuko Letu Blog, na Native Films.

   NB;- Unaweza LIKE page yake LIL STIGGAR kupitia facebook kwa jina la LIL STIGGAR na instagram kwa jina la LILSTIGGAR. 

Imeandikwa na Chris Bee.
 
Top