Menu
 

Rapper wa kike toka Tanzania Corrine Mary a.k.a Cindy Rulz ametajwa kuwania tuzo za Underground Music Awards (UMA), zinazotelewa nchini Marekani.
Cindy Rulz ndiye msanii pekee wa kike aliyetajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu katika kipengele cha ‘Best International Artist’ akichuana na Joe Young, Apollo &Escobar na Fill Straughan.

Tuzo hizo zimelenga katika kuutambua mchango wa watayarishaji wa muziki, wasanii na waandishi wa nyimbo wasiofanya kazi chini ya label.

Upigaji kura unaanza August 10. Endelea kutembelea tovuti hii.
 
Top