Rapper INSPECTOR
HAROUN amedai Wasanii wakongwe hawashindwi kubuni mbinu mpya za kiushindani
katika muziki na badala yake wanafanya muziki unaoishi hali inayowafanya
washindwe kuwa na utaratibu wa kuachia ngoma mara kwa mara.
"Ukiwa kimya
mashabiki wanahisi umeishiwa, sisi hatutaki kutengeneza muziki wa Big G, sisi
tunatengeneza muziki unaoishi hatutengenezi muziki wetu kwa siku moja au mwezi
mmoja au kila baada ya nusu mwezi kuachia ngoma. Muziki unaoishi unatakiwa
uutengeneze ndani ya miezi kadhaa halafu maproducer tofauti tofauti wanakaa na
kufanya kitu kizuri". alisema hayo kupitia Kipengele cha Chumba Cha
Sindano cha Bomba FM Mbeya na Chimbuko Letu Blog.
Akiendelea na
utetezi wa kauli yake Hitmaker huyo wa Pamba Nyepesi Inspector Haroun amesema
"Kuna kitu ambacho mashabiki wa muziki kwa sasa wanakimiss, sawa wadogo
zetu wanafanya vizuri, wanaimba vizuri wapo wengi wananyakua Tuzo na wengine
wanaishia kuwa nominated lakini hawana uhalisia ukimsikia msanii huyu anafanana
na msanii fulani unashindwa kuwatofautisha".
Kinywa cha Mzee
kinanuka ugolo lakini kinatoa maneno ya busara Inspector Haroun anatoa ushauri upi kwa wasanii wa
sasa? "Kikubwa wasanii walioingia katika gemu ni kuzingatia identity yao,
uwepo wao wautambue unatakiwa kuwa kama wewe, wakati unapoanza muziki lazima
utadokoadokoa sehemu ili upate njia yako ukishapata unatengeneza mfumo ya
kujulikana kama wewe ndio maana sasa hivi AY, Juma Nature, Prof J, Afande Sele,
Jay Moe na wengineo wanajulikana kama wao".
Hata hivyo amewaomba mashabiki wake kukaa mkao wa
kula kungojea video ya wimbo wake uliokamilisha Albamu yake ya Sharubu za Babu
uitwao Mungu Anapanga aliomshirikisha Juma Nature na kupikwa katika studio za
Uprise Music chini ya producer Dupy.
Kupata uhondo BOFYA HAPA