Menu
 

Hitmaker wa So Crazy MAUA SAMA amesema hategemei Scandal katika maisha yake binafsi na kimuziki ili kwa lengo la kupata umaarufu wa haraka usiokuwa na maslahi.''Aaaa!! upande wangu mimi Maua Sama nachukia sana Scandal, naamini kwamba na provide nyimbo nzuri ambazo zinawavutia na zitaendelea kuwavutia ma-fans wangu si kwa kutegemea scandal kupata mafanikio katika music industry'' Alichanika hivyo kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano katika kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.Maua Sama amesema kila siku humuomba Mwenyezi Mungu amuepushe kabisa na suala la scandal ili kukamilisha malengo yake kama kioo cha jamii.''Yaani sipendi kabisa kuwa magazetini kila siku, niko very against napenda niwe kwenye magazeti in a good way lakini not kwenye scandal sababu i like doing things different i mean sijui kama niko different na wasanii wenzangu kutokana na mazingira niliyozaliwa Scandal ni kama aibu kwangu na my family''.


Maua Sama amesema anashukuru mpaka hapa alipofikia kwa sababu promo tu ya muziki imemfanya apate mashabiki wengi.

Kwa habari kamili BOFYA HAPA
 
Top