Menu
 


Muigizaji maarufu wa Marekani Robin Williams, 63, amekutwa amekufa, katika kile kinachodhaniwa kuwa ni kujiua, wamesema polisi wa California. 

Polisi wa kaunti ya Marin wamesema alitangazwa kuwa amefariki muda mfupi baada ya maafisa wa polisi kwenda nyumbani kwake baada ya kupigiwa simu ya dharura. 

Williams alipata umaarufu katika filamu kama Good Morning Vietnam, Dead Poets Society, Mrs Doubtfire, na hata kushinda tuzo ya Oscar katika filamu ya Good Will Hunting. Wakala wake amesema mcheza filamu huyo alikuwa akipambana na "msongo wa mawazo". 

Siku za nyuma, aliwahi kuzungumzia, na hata kufanya mzaha, kuhusu anavyosumbuliwa na mwenendo wake wa kutumia dawa za kulevya na pombe.

 Williams alikuwa amerejea katika kituo kimoja cha afya hivi karibuni kujaribu kurekebisha mwenendo wake huo, liliripoti gazeti la Los Angeles Times mwezi Julai. "Kwa wakati huu, ofisi ya liwali, idara ya vifo inadhani kifo hiki huenda ni cha kujiua kutokana na kukosa hewa ya oksijeni, lakini uchunguzi kamili lazima ufanyike kabla ya jibu la mwisho kutolewa." polisi wamesema katika taarifa yao.
 
Top