Menu
 

Siku moja baada ya kusajiliwa na mabingwa wa soka barani Ulaya, Real Madrid akitokea kwenye klabu ya Levance kwa ada ya uhamisho wa Euro million 10, mlinda mlango kutoka nchini Costa Rica, Keylor Antonio Navas Gamboa, amependekezwa kuwa chaguo la kwanza la meneja Carlo Ancelotti.

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wasomaji wa mtandao wa AS.com, mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27 wameshauri suala la kufanywa kwa mabadiliko katika lango la Real Madrid kwa kuamini Navas anafaa kwa sasa.

Kwenye mtandao wa AS.Com swali lilikuwa limeulizwa kwa wasomaji juu ya mabadiliko ambayo yanatakiwa kufanywa katika lango la Real Madrid asilimia 52.99 ya wasomaji wamependekeza Navas kuwa chaguo la kwanza zaidi ya mkongwe Iker Casillas.

Mpaka taarifa hizi zinachapishwa katika mtandao huu, wasomaji zaidi ya 23,000 walikuwa wameshapiga kura na kumpendekeza Navas kuwa chaguo la kwanza huku wakiamini ana uwezo wa kuilinda Real Madrid kwa umakini zaidi ya Iker Casillas ambaye kwa miaka miwiwli iliyopita ameonekana kuporomoka kiwango.

Mbali na kuonekana si lolote kwa Navas kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandai wa AS.com, bado Casillas ametupwa katika nafasi ya tatu ambapo mpinzani wake kwa sasa mlinda mlango kutoka nchini Hispania Diego Lopez amepata asilimia 29 ya kura hizo.

Asilimia 17.71 zimekwenda kwa Casillas ambaye imeshaanza kutabiriwa huenda akapata wakati mgumu wa kujihakikishai nafasi kwenye kikosi cha kwanza kuanzia msimu ujao wa ligi.

Credit:- Times FM
 
Top