Menu
 

Hitmaker wa Lofa TOP C amemaliza malumbano yaliyokuwa yakimkabili na Menejimenti yake ya Candy n Candy Records ya nchini Kenya, kutokana na menejimenti hiyo kushindwa kutekelezea maadhimio ya mkataba wao.

TOP C amesema makubaliano waliyoyafikia namenejimenti yake hiyo ni maslahi ya mapato ya nyimbo zake, kufanyiwa promotion, kurekodi nyimbo na kuzifanyia video pamoja na kuandaliwa show.

"Walinipigia simu tukafanya maongezi, wamekubali kunifanyia nitakavyotaka, kama mkataba unavyosema hivyo wamehitaji nirudi kwenye kampuni na nilitakiwa niwenimekwenda Nairobi lakini nilikuwa na matatizo ya kifamilia kwa hiyo mwezi wa tisa nitakuwa huko kuendelea na shughuli za kimuziki chini yao". Alifunguka kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano cha redio Bomba FM Mbeya na Chimbuko Letu Blog.

Hata hivyo ameelezea manufaa yatakayoanza kutekelezwa moja kwa moja mara baada ya kufika Nairobi "Nipo mbioni kuachia video ya wimbo wangu wa Nihurumie hivi punde chini ya usimamizi wao, lakini pia kuna ngoma nyingine itafuata itaitwa kisura, ambayo mpenzi alitoka home Tanga kuja Dar es salaam kunitafuta mwisho wa siku hakunikuta mimi sikuwepo akapangishiwa ghetto na wanawake wenzake na kuanza kutumikishwa katika biashara ya ngono". Kupata uhondo BOFYA HAPA
 
Top