Menu
  

Hitmaker wa Mfalme wa Temeke Young Tuso ameweka bayana kuwa wasanii wenzake AY na Diamond Plutnumz ndio wanaomfanya ashindwe kuzifanyia nyimbo zake video.

Amedai kuwa ukubwa wa video zao(ubora wa video) zenye ushindani wa kimataifa humfanya aone muziki wake kuwa wakibiashara,kutokana na kushindwa kumudu gharama za kutengeneza video zenye ubora huo kwa sababu ya kutokuwa na menejimenti.

''Labda mashabiki waelewe kama wanavyojua muziki sasa hivi umeshakuwa wa biashara, watu sasa hivi wanaenda Marekani, South Africa kwenda kushoot video za nyimbo zao ili mradi watengeneze kitu chenye ubora, muziki wao ufike mbali na mashabiki wa muziki waendelee kushawishika kuzitazama'' alisema Young Tuso kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano katika kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Kwa upande mwingine Young Tuso amesema ''Sababu hizo ndizo zimekuwa zikinifanya niwe mwoga kutengeneza video isiyokuwa na ubora au haitakidhi viwango, nipo katika mazingira ya kujipanga ili nije nitengeneze kitu ambacho kitakuwa na mashiko''.
 
Top