Menu
 
Hitmaker wa Jichunge ambaye pia ni mzawa wa Mwanza BARAKA DA PRINCE amepinga kuwa si muziki wa Hip Hop tu una uhalisia bali hata aina nyingine ya muziki ina uhalisia kuishi vilevile bali tofauti ipo katika ubunifu wa mashairi mapya.

''Kuna mtu atatuambia kuwa sisi tunaimba muziki ambao hauna uhalisia wa maisha? Hapana tunaimba vitu ambavyo vinatokea tunatofautiana ujumbe tu ila kila tunachokiimba kinatokea katika jamii'' Alisikia BARAKA DA PRINCE kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.Aidha BARAKA amewashukuru mashabiki wake kumpokea vizuri katika gemu la muziki'' Watu wanapokea vizuri, tofauti na mimi navyotegemea hata show nazofanya najua kabisa daaaah! kweli nasema nafanya kitu zinanipa ripoti nzuri. Mwanza ujue ni nyumbani naweza kusema Rais mimi kule, wewe kama ni mfuatiliaji unkiangalia kwenye mitandao, kwenye TV hata kwenye show za FIESTA ukiona hata show ya kule utajua mimi ni mtu fulani kule''.
 
Top