Menu
 
Mwanamuziki Linex Sunday Mjeda ameamua kuwatumia utaratibu wa kuwaimbisha zaidi mashabiki nyimbo zake kwenye show mbalimbali ili kujiwekea hazina ya kukumbukwa mara kwa mara na mashabiki wake.''Asilimia 100 nafikiri nimekuwa nikiongea kuwa sasa hivi show yangu nimekuwa sifanyi pekee yangu  nafanya na wahusika ambao wanakuwa pale, yaani tuna-share happiness kwa sababu mimi hata napokuwa naimba hata moyo wangu ukiwa na feelings lakini moyo wangu huwa unakuwa free na ninafurahi popote uliko lazima ujue unakuja kushare furaha na mimi kwa hiyo unakuja kuimba na mimi'' Linex ameiimbia Bomba FM ya Mbeya.Hata hivyo amezungumzia sababu ya nyimbo zake kupendwa zaidi na Mabinti. ''Sio mabinti tu watu wote unajua rekodi zangu zina kitu fulani ambacho kipo really, unajua siku zote ukweli huwa haufichiki. Kwa sababu ukiangalia Mama Halima kuna watu watukio yale wamekutana nayo au vipi walikuwa na wapenzi yakawa moja mbili tatu, zile Moyo wa subira ukiangalia ni ngoma fulani ambazo zimerudisha mahusiano ya watu au watu walikuwa wakigombana na watu wao makazini na nini  wanatumia yale mashairi kurekebisha mahusiano yao ina wahusu watu wote by the way''.
 
Top