Menu
 
Hitmaker wa 'Basi Nenda' MO MUSIC amesema mipango mizuri aliyokuwa nayo toka awali ndio imeifanya ngoma yake kuwa kubwa na kutochokwa mapema na mashabiki wa muziki Bongo.''Unajua kila kitu kinakuwa na mipango, ukifanya kila kitu kwa strategises lazima utafika katika malengo yako, Kwa hiyo basi nenda ilikuwa na mipango kabla haijatoka kwa hiyo mipango mizuri imesababisha basi nenda kuwa kubwa kiasi hiki''. Alichanika hivyo MO MUSIC kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.MO MUSIC ameongeza kwa kusema ''Nipende kusema nawashakuru sana mashabiki kwa kunipokea vizuri, sijui ni kona gani ambako track hii haifanyi vizuri sio mtoto sio nani. Kwa hiyo naweza kusema MO MUSIC wasimtegemee sio yule anaye fanya nini, MO MUSIC naweza pia kurap''.Hata hivyo MO MUSIC amekiri kupata upinzani mkubwa katika gemu la muziki wa kipazi kipya jijini Mwanza kutoka kwa msanii mwenzake BARAKA DA PRINCE ambaye ni mzawa wa jijini humo. ''Kila mtu anamwonekano wake na mtizamo wake na reality inaonekana any way anafanya vizuri BARAKA, nafanya vizuri kwa upande wangu''.

BOFYA HAPO CHINI KUSIKILIZA
 
Top