Menu
 


Jana usiku bondia Floyd Mayweather alizichapa ulingoni na Marcos Maidana, MGM Grand Garden Arena, Las Vegas, Marekani.

Kwa mara nyingine, Mayweather ameutetea mkanda wa ubingwa wa dunia kwa kumshinda Maidana kwa mara ya pili kwa points zilizozua hisia tofauti. 

Majaji walimpa Floyd ushindi wa points 115-112, 116-111 na 116-111 baada ya kukamilika kwa rounds zote.

Hata hivyo, Floyd Mayweather aliweka wazi kuwa pambano hili lilikuwa gumu zaidi kwake kuliko pambano lao la kwanza.

“I felt I did better in the first fight. This fight I felt dry and dead.” Alisema Mayweather.

Naye Maidana anaamini kuwa yeye ndiye mshindi wa pambano hilo ingawa majaji walimpa Floyd.

“I thought I won the fight, but if the judges want to give it to guys who run, that's how it is.” Alisema Maidana baada ya pambano.

Matokeo ya jana yanamfanya Mayweather kuendelea kuweka rekodi ya kutopigwa katika mapambano 47 aliyopigana.

 
Top