Menu
 

Mwanamuziki wa jumba la vipaji Tanzania(THT) RECHO amesema kujitambua kwake ndio njia kuu inayomfanya asiteteleke katika muziki kutokana na kuutegemea zaidi katika kupata kipato cha kuendeshea maisha yake.''Siri kubwa nikujua ni kitu gani unakifanya, kwa sababu kuna mtu mwingine anakuwa anafanya halafu hajui kitu gani anakifanya, yaani hajielewi yuko wapi? Mimi ninafanya muziki halafu muziki ndio maisha yangu''. Alichanika hivyo RECHO kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.Aidha RECHO amesema anategemea sana Muziki umpe mafanikio na jina kubwa ila si kwa skendo. ''Mimi nategemea muziki, unajua skendo iko hivi unaweza ukatoka kwa skendo lakini skendo hiyo hiyo inaweza ikakudondosha vile vile''.KIPAJI ANAKIDHIHIRISHA VIPI:- Je, humchukua muda gani kuandika ngoma zake?  Kiukweli nyimbo zangu nyingi huwa siandiki yaani huwa inatokea studio hapo hapo, huwa napenda kuinbgia studio na kuanza kufanya kazi. Muziki ujue ni Mood mtu hawezi akuamsha asubuhi akakuambia uende studio na usifanbye kitu chochote ukiwa hauna mzuka huwezi kufanya kitu'' alisema RECHO.

BOFYA HAPO CHINI KUSIKILIZA

 
Top