Menu
 Mwanamuziki wa miondoko ya RnB Bernad Paul a.k.a Ben Pol amesema uamuzi wake wa kuwalipisha pesa wasanii wachanga wanapomhitaji kumshirikisha katika ngoma zao kwa sababu husafiria nyota yake.


“Underground namlipisha kwasababu, samahani kwa kutumia neno hili anakuwa anakutumia, yaani wimbo unavyokuwa fulani featuring Ben Pol hili jina la Ben Pol nimelitumia vitu vingi na gharama nyingi mpaka kuwa Ben Pol ushanielewa kwa hiyo kwa hatua niliyokuwa nayo naye msaniii mchanga ataitumia kama fimbo ili atoke kwa kawaida hawezi kukulipa gharama zote mpaka ulipofika na lakini pia angalau tufanye biashara kuwa serious lazima achangie kitu Fulani na wimbo pia uwe mzuri” Ben Pol alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Aidha Ben Pol ameelezea sababu zinazomfanya amlipishe pesa ya Collabo msanii mchanga tu na kutowalipisha wasanii wakonge, “Kwa kipindi hiki Collabo nimesitisha, yaani kuna zile collabo za kulipwa na zile za connection. Kwa mfano mtu kama FID Q huwezi kumwambia akulipe ufanye naye kazi au akitaka upige chorus lakini mbali na hapo msanii mchanga akinitaka nifanye naye collabo asubiri mpaka mwezi wa pili sasa hivi labda aje kwa kutaka ushauri tu muda wowote nafanya bila gharama yoyote”.
 
Top