Menu
 Rapper One Incredible anatarajia kuiachia albamu yake ya pili inayokwenda kwa jina la R.A.P(Representing Africa Popote) Desemba 5 mwaka huu.


“Harakati zinaendelea kama kawaida na tarehe 5 Desemba natarajia kuachia albamu ya pili yenye ngoma 15 na inakwenda kwa jina la Representing Africa Popote yaani RAP” alifunguka One Icredible kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Awali albamu hiyo ilitarajiwa kutoka Novemba 6, mwaka 2013 na hapa anaelezea uamuzi wake wa kuiachia Albamu hiyo Desemba 5 “Sasa hivi nina management mpya nimefungua kampuni yangu mpya ambayo inasimamia kazi zangu, ndio kitu kilichofanya albamu yangu niisongeze mbele. Ni mafanikio mengi nimeanza kuyaona toka nikiwa na management mpya lakini nisingependa kuyaongelea kwa sasa”.

“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula albamu yangu imepikwa na Maproducer tofauti tofauti akiwemo Mjwauki ambaye alikuwemo katika albamu yangu ya kwanza, Nikki Mbishi, mimi mwenyewe One, Dunga wa Mandugu Digital nk” alimalizia kwa kusema hivyo Rapper One Incredible.
 
Top