Menu
 Mkoa wa Mbeya unaendelea kukabiliwa na tatizo la utoro na mimba kwa wanafunzi, licha ya Serikali kuendelea na mpango wake wa kuwarudisha wanafunzi waliokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu mkoa wa Mbeya  Remigius Ntyama jumla ya wanafunzi 6,350  wamekatika masomo kutokana na tatizo la ujauzito na utoro.

Amesema kati ya wanafunzi 6,302 wa shule za msingi wamekatisha masomo kutokana na utoro na wanafunzi 6 wamekatisha masomo kwa ujauzito.

Aidha amesema kati ya wanafunzi 4,631 wa shule za sekondari, ambao wamekatisha masomo yao, wanafunzi 4,418 wamekatisha masomo kwa sababu ya utoro, wanafunzi  69 kwa sababu ya ujauzito na 44 kwa sababu ya vifo.

Wakati huohuo amesema hadi kufikia Septemba 30 mwaka huu jumla ya wanafunzi 138 wa shule za msingi na wanafunzi 94 wa sekondari ambao walikatisha masomo kutokana na sababu hizo walirudishwa shuleni..
 
Top