Menu
 Mkali wa miondo ya Miduara nchini AT amesema wasanii watazania wanaokimbilia kufanya video za nyimbo zao Afrika Kusini ni malimbukeni na washamba wa kubwa kutokana kutangaza rasilimali za nchi hiyo badala ya kutangaza rasilimali za Tanzania ili kuwavutia wageni kutembelea nchini na kuongeza pato la taifa.

''Kikubwa ambacho nimekuwa nikikifanya ni kufanya video tofauti, wasanii wa Tanzania wamekuwa washamba sijapata kuona, malimbukeni duniani hakuna unawezaje kutoka nchini kwako ukaenda kumpromote Msouth Africa ni kwa sababu ya majengo hata siku moja tunajidanganya bora upeleke chako watu wakiona. Wimbo ambao unampa heshima msanii John Legend mpaka kesho ni video aliyoifanyia Zanzibar, na John Legend kwao Marekani hivi alikosa kazi mpaka kufanyia video kule Zanzibar si Tanzania kwanini tusiwe wazalendo, tunataka Serikali iwe na uzalendo au Wananchi wawe wazalendo kutusaidia sisi wasanii watanzania mbona sisi sio wazalendo kwa nchi yetu'' AT alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

''Mimi sina mpango wa kufanya video South Africa, mimi sio mshamba wa majengo, vioo navijua na majengo nayajua Posta pia yapo ndio yale yale ila sehemu tofauti tu ni mpangilio, lakini tunapokuja kwenye suala nzima la Rasilimali atazipeleka nani zijulikane ziwavutie watu waje hapo ndio tunapochemka. Tukiangalia Filamu za Kimarekani hivi ulishaona Sterling wa kimarekani kapingwa, Mmarekani anaweza akaingia sehemu China akapingwa na akatoka pekee yake ile ni kutangaza Taifa lao lionekane lina nguvu kwa kuwafanya watu waamini kuwa wananguvu zaidi wanatangaza chao zaidi lakini sisi tumeshindwa kutangaza chetu'' aliongeza AT

Aidha AT amewataka wasanii hao kuacha tabia kuwakejeli Ma-Director wa video wa Tanzania kwani nao wameleta changamoto kubwa ya mafanikio kwao ''Tumeanza kuwa-kashfu akina Adam Juma, Nisher na watu wengine kwamba video zetu hazina ubora mbona wakati tunaanza kufanya video hatukuenda South Afrika  kufanya kwa sababu tumetoka leo hii tumekuwa hatuna shukrani suala la nyimbo za Tanzania hatakuja mtu kusema mie nawasaidieni, hakuna Mnigeria atakuwa na roho ya huruma na Tanzania wala Msouth Africa isipokuwa Watanzania wenyewe watakuwa na imani na vitu vyao wenyewe''.
 
Top