Menu
 

Mwanamuziki wa miondoko ya miduara nchini Tanzania AT anatarajia kumtambulisha mdogo wake aitwaye Nasir lakini jina la kisanii ni Vanilla kupitia wimbo anaotarajia kuuachia Januari 15 mwaka huu.

''Tarehe 15 nitakuwa naachia wimbo wangu mpya uitwao 'Mama Mamie(unanipenda)' ambao utakuja na video yake sambamba na utambulisho wa mdogo wangu aitwaye Vanilla ambaye nimeona muda wake wa kufanya muziki sasa umefika na anaweza kuleta pirika'' AT alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

''Mdogo wangu ana uwezo wa kufanya muziki wa Bongo Fleva, miduara lakini ana muziki wake ambao unajitambulisha wenyewe kama wenyewe haufanani na muziki wa msanii yeyote, lakini watu wanaamini muziki ni uleule lakini muziki si uleule isipokuwa code za muziki ni zilezile unaweza kutengeneza muziki mzuri endapo ukiwa unajiongeza kufikiri ndio kilichojidhihirisha kupitia kwa mdogo wangu''.
 
Top