Menu
 Mwanamuziki anayetamba na ngoma ya Katapila BABY J amesema ongezeko la wasanii wa kike kila siku katika music industry ndio sababu kuu inayomfanya kujikita katika kufanya aina tofautitofauti ya muziki kama Mduara, Regge na Bongo Fleva.

''Hii yote najiamini najua nauweza muziki na mimi ni mwanamuziki wa ukweli kabisa, kwa hiyo najaribu kuonyesha watu kwamba mimi naweza kufanya style yoyote ya muziki na ikafanya vizuri kwa sababu nimeshafanya Regge, Mduara, Zouk/Bongo Fleva na aina nyingine za muziki na zikafanya vizuri kwa hiyo ni baadhi tu ya radha nayo wasogezea shabiki zangu wajue kitu gani naweza kufanya'' alikiambia Kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Aidha BABY J amesema haina budi kwa wasanii wenzake wa kike waliopo muda mrefu katika gemu la muziki kuongeza ubunifu wa kufanya aina tofauti tofauti ya muziki ili kuendana na ushindani baina yao na wasanii wachanga.

''Kundi la wasichana wanaofanya muziki wa aina kama yetu kwa hiyo na sisi tuliopo muda mrefu katika tasnia ya muziki tunazidi kujipanga vizuri, tunazidi kuwa katika ushindani itafanya waamini kuwa wanawake nasi tumeamua au Baby J naye ni miongozi mwa wasanii wanaofanya vizuri''. alisema BABY J

Hata hivyo BABY J yupo katika harakati za kukamilisha Video ya wimbo wa Katapila anayofanya na Director mkongwe Adamu Juma.
 
Top