Menu
 Hitmaker wa Jikubali 'Bernad Paul a.k.a Ben Pol' amesema malengo yake ya mwaka 2015 ni kulifikia soko la ushindani la kimataifa katika muziki wa kizazi kipya, kunyakua au kuwa nominated katika tuzo za kimataifa pamoja na video za nyimbo zake kuchezwa katika Luninga za Kimataifa.

''Bado tunaendelea kupambana, bado tunaendelea ku-push kazi ninaamini siku moja Mwenyezi Mungu siku moja nitakuja kutokezea sehemu, kwa hiyo tayari nimeanza kutumatuma nyimbo kama kwa mwaka jana nimeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani mpaka kupata nomination kwenye tuzo za AFRIMMA kupata aittime kwenye International TV Stations kwa hiyo taratibu taratibu ninaendelea. Mwenyezi Mungu akajaalia mwaka huu tena nitapanua network kidogo na kufanyafanya collabo na wasanii wa kimataifa vitu vikaa onset nafikiri tutapeana taarifa'' BEN POL alikiambia Kipindi cha Bomba Base Show ya redio Bomba FM Mbeya.

Akiizungumzia ngoma ya SOPHIA aliyoiachia hivi karibuni BEN POL amesema ''Mimi naamini kwamba bado unaweza kufanya kitu vyovyote vile vile kitu kinachomata zaidi muziki mzuri, ukaimba vizuri, ukaandika vizuri, meseji inasemaje, melody ikoje, haijalisha title ya wimbo imekaaje na title ya wimbo nadhani ni kitu ambacho kinasapoti kwa hiyo na hata huo wimbo sio kwamba namwimbia Sophia nakupenda hapana ni wimbo ambao upo tofauti ni wimbo ambao nimezungumzia uzuri wa Tanzania, uzuri wa Dodoma ninakotokea na Uzuri wa Afrika’'.

Hata hivyo Ben Pol ameweka bayana namna ya kuaziachia kazi zake mpya kwa mwaka huu wa 2015 ''Kwa mwaka huu tutegemee na uhitaji wa watu naweza nikapanga kutoa nyimbo tatu au nne kwa mwaka, halafu ukatoa nyimbo mbili au wimbo mmoja ika-hit zaidi mwaka mzima kwa hiyo hapo unakuwa hauna jinsi au ukatoa nyimbo mbili zikakubana mwaka mzima zikawa zinazunguka watu wanaziomba huku, wanazitaka, wanahitaji show''.
 
Top