Menu
 Rapper Bonta amesema mashabiki wanapaswa kufahamu sisikiki kupitia ngoma za Weusi kwa sababu huwa nakuwa nipo kwenye majukumu ya ndani na nje ya nchi kutokana na taaluma yangu ya udaktari.

''Mara nyingi mimi nakuwa sipo unajua kwa mfano kama mwaka jana kwa miezi 12 nilikuwepo nchini kwa miezi minne tu, na miezi minne yenyewe ilikuwa ya mwisho mwisho wakati tunafanya tour ile ya Funga Mwaka na Weusi ndio nilirudi mwezi wa 8 na hata nikiwepo nchini mara nyingi nakuwa mikoa ya Mwanza, Arusha na Shinyanga nacheza na hiyo triangle na wenzangu wanakuwa Dar es Salaam lakini na mchango mkubwa katika kazi zote za weusi'' Rapper Bonta alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Bonta pia amezungumzia mafanikio ya Kampuni yao ya Weusi kuwa mwaka 2014 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwao.

''Ulikuwa ni mwaka mzuri kwa kampuni yangu ya weusi tumefanya vizuri kwenye TV, Radio stations, shows na hata mtaani kwa kusikilizwa sana kwa sisi wasanii watano wa Weusi pekee yetu tumetoa video 8 kwa hiyo ni jambo la kujivunia''
 
Top