Menu
 Rapper Chiku Keto amesema haelewi sababu za Mameneja wengi sasa hivi kutokuwa tayari kuwasimamia baadhi ya wasanii wanao-rap.

Chiku K ameyasema hayo katika Kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya, wakati akizungumzia sababu za ukimya wake kwa 2014 katika music industry ulitokana na harakati zake za kutafuta menejimenti na mtu yoyote ajitokeze kusimamia kazi zake.

''Kilichokuwa kinanikwamisha nilikuwa nasikilizia kama labda inaweza ikatokea mtu ambaye anaweza kunisimamia kazi, sielewi watu kwanini wamekuwa wagumu wanakuwa hawajitokezi kwa hiyo nimeamua kusimama mwenyewe vyovyote itakavyokuwa itabidi nifanye kazi yeyote mtu akiona unaelekea basi atasapoti''.

Hata hivyo amezungumzia kuanza na ngoma yake mpya atakayoiachia maalumu kwaajili ya sikukuu ya wapendanao kama zawadi kwa mashabiki.

''Nachowaambia narudi sasa hivi nakuja tarehe 14 mwezi wa pili mwaka huu siku ya Valentine naangusha ngoma vyovyote itakavyokuwa hapa napiga picha ya cover ya wimbo huo unaitwa Usiniache ni wimbo fulani hivi wa mapenzi nimerap na nimeimba''
 
Top