Menu
 

Mwaka 2014 ulikuwa ni mwaka wa mipango kwa msanii Dayna Nyage kufanya collabolation na msanii Cindy kutoka nchini Uganda lakini mipango hiyo haikukamilika kutokana na msanii huyo wa zamani wa kundi la Blu 3 (Cindy) kupata safari za mara za kuelekea Afrika Kusini.

''Kila kitu kipo vizuri, wakati mwingine sisi tunaweza tukawa tunapanga vitu lakini na Mungu anakuwa anapanga vya kwake, kwa hiyo kama binadamu lazima tukubali kuwa na subira tu na ukiangalia Uganda ilikuwa ni karibu tu ilikuwa ni rahisi mimi kwenda kukaa siku mbili tatu na kufanya wimbo na ukakamilika''. Dayna Nyange alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

''Lakini kwa mara ya mwisho kuna vitu vilitokea upande wa pili, tulikuwa tayari kufanya mara kadhaa nilipanga kwenda Uganda, Cindy akapata tena safari ya ghafla kwenda Afrika Kusini kwenye tuzo, kwa hiyo tukawa tumepisha ila kwa sababu na mimi nilikuwa na majukumu mengine nikaamua kutulia kwanza nimalizie mambo yangu'' alisema Dayna.

Hata hivyo Dayna amesema mipango ya kufanya collabo na Cindy ipo pale pale na wakati wowote mwaka huu itakamilika ''Kwa hiyo kuna vitu vingi vina kuja na mimi na Cindy ni watu wa karibu sana, tunawasiliana na kukumbushana kuhusu kazi ya pamoja''

 
Top