Menu
 Hitmaker wa Mida ya Kazi DULLAYO amesema muziki wa Bongo Fleva tuliokuwa tunaupigania ukue kimataifa ndio huu na matunda yake yameanza kuonekana ndio maana wasanii wanakwenda kurekodi nyimbo na kushoot video zao Afrika Kusini.

''Unajua muziki wa sasa hivi tofauti na wazamani ulivyokuwa watu hawakufikiria kama wasanii wa Bongo wangefikia huko kwenda kufanya video huko, hii inaonyesha jinsi gani muziki unaonekana unalipa, kama mtu unatoka unaenda kufanya na Godfather na madirector wengine maanake umejipanga vizuri unajua biashara iko wapi na inaleta chachu ya Madirector wa kibongo kufanya kazi kwa bidii kwani wakifanya vibaya watahofia soko lao kuwa gumu, kama wasanii wanaanza kuchukua ndege na kwenda huko hata mimi nitaacha kufanya video huku''. DULLAYO alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Aidha Dullayo amekiri kufanya video na Madirector wa Tanzania hakusaidia kutambulika kimataifa kutokana na kukosa connections za kujitanua kimataifa,

''Unajua wale jamaa wa nje ya nchi wanakuwa na vituo vyao vya luninga wanavyoweza kukusaidia kuisambaza video yako ndio maana unakuta siku hizio wasanii wetu wanakuwa nominated katika tuzo mbalimbali za kimataifa na kuzinyakua tuzo hizo, pekee yetu tu hatuwezi kufika popote ndio maana tulikuwa tunatumia mpaka Channel O watu wanashangaa kwa vyovyote Directors wa nje wanamchango mkubwa''.
 
Top