Menu
 Mwanamuziki na Mwigizaji wa Filamu nchini Frola Mvungi ambaye jina la kisanii kupitia muziki anafahamika kama H MAMA ameipongeza familia yake hususani mumewe ambaye pia ni mwanamuziki H BABA na Mama Mkwe wake kwa kushirikiana vizuri katika malezi ya mwanae Tanzanite.

H MAMA amekiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya kuwa licha ya yeye na mumewe kujikita katika muziki na filamu lakini mtoto wao hajawahi kuteteleka kiafya na analelewa katika misingi na maadili yanayofaa.

''Kabla ya kufanya kitu chochote unajua kuna mipango na malengo, kiukweli nashukuru sana familia yangu kwa sababu wananipa sana sapoti including my husband na Mama mkwe wangu, kwa hiyo mara nyingi navyokuwa nimeenda kushoot ama kufanya show Tanzanite anakuwa na bibi yake all the time so hata mimi huwa nakuwa vile na amani mtoto yupo kwenye mikono salama kwa hiyo hilo hakuna tatizo na vilevile na mdada ambaye anampenda sana mwanangu Tanzanite'' alisema H MAMA.
 
Top