Menu
 

Hitmaker wa 'I Love U' Kassim Mganga awaomba radhi mashabiki wake kwa kuchelewa kuiachia video ya wimbo ya I love u kutokana na kuahidi kuiachia mwishoni mwa mwaka 2014.

''Ratiba ni muda, unajua muda ulikuwa mdogo kwangu, mara nyingi kwa mwaka naachia wimbo mmoja pamoja na video, sasa mwaka jana sikufanya kabisa video ya I love u licha ya kuahidi kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu sambamba na kuwa na show nyingi sana mwaka jana pamoja na safari ya Marekani'' Kassim Mganga alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Kassim Mganga amesema kutokana na sababu hizo lakini kulikuwa na video ya wimbo wa Motomoto iliyotengenezwa na kampuni ya video ya nchini Kenya, Ogopa DJz ambayo ilitakiwa kuwa mbadala wa video ya I Love U lakini alishindwa kuiachia kutokana na kuwa na mapungufu kibao.

''Mwishoni mwa mwaka tukasema tu-release wimbo wa Motomoto na tulianza kushoot video yake kabla ya kurelease wimbo huo, tulishoot na Ogopa Video kutoka nchini Kenya na baadae video tulivyotumiwa haikuwa kama vile tulivyotaka iwe ilikuwa na mapungufu kibao kwa hiyo tukawaambia jamaa inatakiwa tuongeze vitu lakini bado haikuwa vile kama tulivyotegemea nikaona ni hasara tena ikabidi niiachie hivyo hivyo pamoja na video nyingine ya Nafsi nyonge niliyoifanya miaka mitatu iliyopita''    

Hata hivyo Kassim Mganga amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kupata ngoma mpya ''Harakati zinaendelea unajua muziki sasa umekuwa biashara kila wakati inabidi kujisogeza kidogo, ili uweze kukimbizana na market kwa hiyo nipo kwenye maandalizi sasa ya wimbo wangu mpya niliomshirikisha Christian Bella utakao toka mwezi wa tatu''.
 
Top