Menu
 

Hitmaker wa So Crazy Maua Sama amesema ukata na kubanwa na majukumu ya masomo chuoni ndio sababu kuu zilizochangia kutotoa video yoyote ya nyimbo zake ambazo ni So Crazy, Sijiwezi na Let them know nk.

''Ni ukosefu wa fedha na majukumu ya chuo sometimes vikwanzo vya hapa na pale na arrangement ndio sababu zilizochangia nishindwa kufanya video yoyote lakini kwa sababu nahitimu chuo mwaka huu Mungu akijaalia nitaanza kufanya video ya wimbo wa Let them know na nyingine za nyuma zitafuata mpaka So Crazy'' alisema Msomi huyo wa Chuo cha MUCCOBs Maua Sama kupitia Kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Maua Sama licha ya kuwa chini ya Management ya Rapper Mwana FA lakini amefafanua makubaliano ya mkataba baina yake na bosi wake ulivyo ''Ananisaidia kusambaza nyimbo zangu kwenye vituo vya redio, mikakati ya video inafanyika lakini tatizo kuu ni kama nilivvyoeleza muda wangu unabanwa na chuo pamoja na ukata wa fedha, lakini naamini nikihitimu tu chuo niambo yote yatakwenda sawa''

Hata hivyo ameelezea malengo yake katika tasnia ya muziki ''Mimi nasoma biashara kwa unatakiwa kuprovide kitu gani kwa muda gani, ujue muziki nao unabadilika, nitakavyokuwa natoa wimbo lazima mashabiki waangalie una ubora upi na kwa muda gani Unajua ukijikita katika aina moja mashabiki nao wanahama ukitaka kufanya muziki biashara inabidi ubadilike kulingana na soko linavyoenda kwa hiyo sio kila siku watasikia RnB napenda niwe nabadilika kulingana na soko''.

 
Top