Menu
 

Msanii wa zamani wa kundi la Tiptop Connection Pingu amesema hana bifu yoyote na viongozi wa kundi hilo Abdu Bonge, Babu Tale wala Madee lakini hali muziki ikiniendea mrama nitaomba msaada wao.

''Mtoto anapokua anaanza kwa kukaa, kutambaa mwisho wasiku anasimamia kitu baadae pekee yake nakuanza kutembea, mimi nilivyokuwa kule nilikuwa kama mtoto nayelelewa na kuishi katika mazingira ya maisha bora, kwa hiyo sasa hivi naishi maisha ya mtaani nakomaa angalau niweze kujitegemea''. Pigu alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Redio Bomba FM Mbeya.

Katikati ya mwaka 2014 Pingu aliachia ngoma inayokwenda kwa jina la Leo leo aliyomshirikisha Nay wa Mitengo na Sheby Love lakini haikufanya vizuri kama alivyokuwa akitarajia.

''Unajua unavyokuwa chini ya usimamizi kuna mambo mengi mazuri unafanyiwa pamoja na kusimamiwa suala promo ya nyimbo, kusambaziwa katika vituo vya redio, kutengeneza video na kuandaliwa shows lakini unavyokuwa pekee yako kuna vitu unafeli lakini mambo yakiendelea hivi kusuasua nitarudi na kuwaomba waendelee kunisimamia ili malengo yangu kutimia''. alisema Pingu.

 
Top