Menu
 Mtayarishaji wa Muziki wa Kizazi kipya LAMAR ameweka wazi kuwa hajaishiwa ubunifu katika utayarishaji wa muziki lakini amefanya kazi nyingi za wasanii lakini hawataki kuziachia hali inayochangia aonekane kuwa kimya katika music industry.

LAMAR amekiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya kuwa ''Siku zote mimi niko tofauti, ujue watu hawaelewi mimi narekodi nyimbo lakini sina mamlaka ya ku-release wimbo wa msanii mpaka artist mwenyewe akubali ndio maana naonekana nipo kimya''.

''Lakini tracks narekodi kama kawaida na zipo bado kwenye library  mpaka msanii mwenyewe awe tayari kui-release ndio naziachia na utazisikia katika redio ndio hapo utajua kuwa mimi nimefanya kazi’' ameongeza Lamar.

Hata hivyo LAMAR amesema kwa sasa hawezi kupanga bei mpya ya utayarishaji wa nyimbo, mapaka atakapoona changa moto za mabadiliko katika muziki kwa mwaka huu ''Gharama zangu zinafahamika ngoja tuone mwaka huu toune changes zitakazokuja nahisi itakuwa surprise kwa sasa ziwezi kusema kitu kabla ya muda wake lakini naomba fans waendelee kuni-support, basically range yangu inapanda kutokana na kazi yenyewe kitu gani nataka kufanya nikitaja gharama halisi nitakuwa nimeji-limit''
 
Top