Menu
 Hitmaker wa Pacha Wangu Rich Mavoko amesema ukubwa wa wimbo huo na video yake imemfungulia milango ya kufahamika na kufanya collaboration na wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki.

''Video hii imenikutanisha na watu wakubwa kibao ambao sijawahi kukutana nao, nimefapa collabo za ndani na nje hapa nimepata collabo na msanii wa Kenya Rabbit ambaye alinitafuta na nimepata collabo na Dr Jose Chameleone na wasanii wengine wakubwa wa Afrika Mashariki ambao sikuwahi hata kukutana nao na nimefanikiwa kukutana nao na kukamilisha malengo'' Rich Mavoko alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Kwa hatu nyingine Rich Mavoko amezungumzia utaratibu mpya wa kuachia kazi zake mpya chini ya uongozi wake unaomsimamia ''Ngoma zipo nyingi tatizo ni muda ambao manejimenti wameupanga wao, umeona kuna nyimbo kama mbili na tayari tumekwisha kushoot na nikipanga kutoa nitawajuza fans wangu kupitia Social networks na media kikubwa naomba sapoti yao waendelee kusapoti muziki wa kitanzania''.
 
Top