Menu
 Mwanamuziki Samir wa Kinyulinyuli amekiri kupoteza mashabiki baada ya kubadili miondoko na maudhi ya nyimbo alizozifanya baada ya Kinyulinyuli.

Akizungumza kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya Samir amesema fikra zake na umamuzi wake unamtuma kufanya nyimbo zake katika miondoko kama ya Kinyulinyuli kutokana na ngoma zake kama Fitina, Nitamchezea aliyomshirikisha Ney wa Mitego kutofanya vizuri

''Kila muziki unakuawa na radha yake na watu wake wa kuwabamba, kuna nyimbo zina hit uswahilini, kuna nyingine zinawabamba watu wazima na kuna nyingine zinawabamba wato wote wa rika tofautitofauti na maeneo tofauti, hivyo uamuzi wangu nataka kurudi katika style za kinyulinyuli na naanza na wimbo ambao nitautoa hivi karibuni'' alisema Samir.

Hata hivyo Samir amepata uongozi mpya utakaokuwa ukisimamia kazi zake iitwayo 69 kwa kushirikiana na Mahewa Entertainment.
 
Top