Menu
 Rapper STEREO amedai anamtegemea zaidi bosi wake  na Rapper AY kukamilisha ndoto zake za kujitangaza kimataifa na kufanya collabo na wasanii wa kimataifa na kwamba mafanikio aliyofikia sasa ni mchango mkubwa kutoka Unit Entertainment.

''Kikubwa ni connections mimi naamini sana connection kwa sababu mimi AY alinikuta tayari mimi nishakuwa Stereo, na ninachokihitaji ni kukua tu kwa hiyo mimi namtumia yeye na nilishamwambia mara nyingi namwambia mimi connections ndio kila kitu nachohitaji, niki come up nikiuliza Ambwene(AY) naomba niende sehemu fulani basi nipeleke huko kama nilivyomuomba kendwa kwa Victoria Kimani basi akanipeleka kwa Victoria kwa hiyo ndivyo nitakavyomuomba niende sehemu nyingine naye itabidi anipeleke huko niende'' STEREO alifunguka kupitia kipindi cha Bomba Base Show ya redio Bomba FM Mbeya.

STEREO amesema ana imani ya kufanikiwa zaidi katika soko la muziki kwani bado ana mkataba wa muda mrefu na UNIT ENTERTAINMENT ''Kikubwa watu wanatakiwa kujua mpaka hapa nilipo kwa mafanikio haya ni UNIT ENTERTAINMENT  ambayo imenipokea kutoka MLAB nilipomaliza mkataba nao. Unit Entertainment na naendelea nayo hadi hapa na nitakuwa nayo kwa muda mrefu sana kwani kuna vitu vingi naona nahitaji kutoka kwa AY''.

Hata hivyo Stereo amesema kuwa yupo katika mazungumzo na wasanii wengine wa kimataifa kwa ajili ya kufanya nao collabo ''Mwaka huu nataka kufanya collabolation angalau 4 za wasanii kutoka Nairobi na Kampala kwa hiyo tumeshaanza kufanya ufuatiliaji na nimeongea na wahusika kuona wanawezaje kuniunganisha nao''.
 
Top