Mwaka 2014 ulikuwa ni wakati muafaka kwa hitmaker wa Nakumis Mis
Timbulo kuuaga ukapela, na huenda ukawa na maswali mengi ni kikwazo gani
kilikwamisha mikakati hiyo kutokamilika.
Timbulo amekiambia Kipindi cha Bomba Base Show cha Redio Bomba FM
Mbeya vikwazo vya kutokamilisha ndoto yake ''Siwezi kusema exactly kuwa kuna
vikwazo lakini wakati mwingine unaweza kupanga halafu muolewaji akazingua ni
vitu vya kawaida, sio sehemu yangu ya kutangaza kwamba niliyekuwa naye ilikuwa
hivi labda angekuwa msanii mwingine angekuwa amesema hadharani na watu
wangekuwa wamesikia yote''.
''Mwisho wa siku huwa naamini kwamba Mungu huwa anapanga halafu huwa
anatia mkono wake kufanikisha hili liende, hili lisiende watu waelewe tu mambo
hayakwenda sawa mimi sio mtu ambaye nachelewesha sana uchumba aua uhawala. Mimi
naamini sana katika Mungu saa nyingine kwa hiyo tunambiwa katika vitabu vya
Mungu kwamba ficheni uchumba tangazeni ndoa'' aliongeza Timbulo
Hata hivyo Timbulo amesema licha ya mikakati kufeli lakini suala la
kuoa lipo palepale kwa mwaka huu wa 2015.
''Suala la kuoa ni mpango endelevu yaani usipooa mwaka huu utaoa
mwakani kama unamini kama mimi ninavyoamini, lakini kwa wale wenzangu ambao
hawaamini kunye mambo ya kuoa na kuishi katika familia hawana ndoto''.