Menu
 Imeelezwa kuwa Wasanii wakongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo ni wanyonyaji wengi wao hupenda kufanyiwa kazi bure bila kulipia gharama za beat au wimbo, hali ambayo husababisha producers wengi kushindwa kufanya nao kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Producer DUPY a.k.a Kono la Chuma kutoka Studio za Uprise Music zilizopo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Kipinchi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Radio Mbeya ''Kikubwa kilichonikwamisha kufanya kazi na wasanii wengine wakubwa ukiwaondoa Juma Nature, Izzo B na wengine.. Wasanii wengi wakubwa wana zile za kujuana mtu anakupigia simu anataka mfanye kazi lakini hazungumzii ishu za malipo au anasema vipi nina mdundo wangu hapo studio sasa hajui kama studio kuna expensive kama umeme nk unakuwa unapigwa kama changa la macho hivi inakuwa majanga lakini ilifikia kipindi nikawa sipokei simu zao''

Hata hivyo amesema yupo katika mikakati ya kuwapa mikataba ya lebo baadhi ya wasanii wakongwe. ''Kwa mwaka huu kuna artists kadhaa ambao nitawataja baadae baada ya kufanya nao kazi ya majaribio tuone mashabiki watawabokea vipi ndipo tuwape mikataba ya lebo''.
 
Top