Menu
 

Rapper WITNESS amesema wasanii wengi wa kike wanaofanya muziki wa Hiphop wanafeli kutokana na kutaka kufanya hiphop kama mwanaume.

Akikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya rapper huyo amesema ''Hiphop yenyewe wanasema dominated game kwamba ni mchezo wa wanaume asili yake iko hivyo unavyokuja mwanamke kutaka kuifanya kama mwanaume unafeli inabidi ufanye kama mwanamke''

WITNESS amesema Female rappers wanapaswa kuiga nyayo za Msanii Nick Minaj, ''kwa mfano kama Nick Minaj anafanya vizuri sasa hivi umemuona she sex halafu vilevile huwa anaimba na anafanya hiphop japo kuwa anafahamika kama mwana hiphop lakini pia kuimba kupo kwa hiyo anachanganya kwa hiyo anatokea kuwa na fans ambao wa kuimba, wanaopenda muonekano wake, anavyoimba, performance zake na wanaopenda Hiphop ndio maana unakuta anavitu kama vitano vinavyomsapoti ndio maana anaendelea kufanya vizuri''

 Aidha Rapper huyo amezungumzia mpango wake mkubwa kwa mwaka huu ni kuachia video moja kila baada ya miezi miwili au mitatu.

''Mwaka huu na mpango wa kuwa natoa video kila baada ya miezi miwili au mitatu, sasa hivi namalizia tu kuisambaza videos ya sasa hivi Chunga mdomo wako ikishaisha naanza kushoot video ya wimbo mwingine''

Hata hivyo WITNESS ameizungumzia video yake mpya ambayo amekwisha kuiachia ya Chunga mdomo wako ''Wimbo mpya nimeuachia unaitwa chunga mdomo wako ni wimbo ambao ukiuangalia au ukiusikiliza utaona kama nimebadilika kidogo nimeimba na kurap at the same time, vilevile  nimetokea kuchange hata kwa muonekano ni video yangu ya kwanza nimetokea kuwa na wanawake tu kwenye video''.
 
Top