Menu
 

Pg.24b
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amedai kuwa kuendelea kuwekwa benchi kwa mlinda mlango wake, Juma Kaseja kumesababisha na yeye mwenyewe.

Hivi karibuni Kaseja hakuhusishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF.

Muro amedai kuwa Kaseja alianza kuwa na kinyongo na Yanga baada ya benchi la ufundi kuanza kumtumia Dida kutokana na kuwa na uwezo zaidi kumzidi kwakuwa katika mechi zilizopita alionekana kushindwa kumudu.

Muro anaamini tatizo lake na Yanga ni kutokana na uamuzi wa klabu hiyo kuamua kuvipa nafasi vipaji vingine kwenye nafasi yake. Kutokana na hali hiyo, hivi karibuni Kaseja amekuwa na mahudhurio hafifu kwenye mazoezi ya timu yake.
 
Top