Menu
 


Hitmaker wa ‘Sherehe’ Baba Levo amedai kukosa udhamini ndio sababu ambayo imechangia kushindwa kuanza kwa ‘TV Reality Show’ ambayo ilitakiwa aifanye na msanii mwenzake Peter Msechu.

“Aaah.. Ile Project ilikwamishwa na ufadhili, kuna problem ilikuwa kati yetu na mtu ambaye anameneji ule mchongo, lakini sasa hivi tupo katika hatua za mwisho mwisho kumaliza hiyo issue na tukimaliza popo zitaamka kusema ukweli” Rapper Baba Levo alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya.

Kwa hatua nyingi Rapper amesema anatarajia kuachia video ya ngoma yake iitwayo Sherehe aliyofanyia nchini Afrika kusini na sababu zilizochangia kuchelewa kuachia.

“Video ya sherehe imeshafanyika na imeshakwisha na imegharimu shilingi milioni 7.3 na nimefanyia nchini Afrika kusini chini ya kampuni ya Kokwa chini ya Benjamin Rushungu, lakini video imechelewa kkutokana na mgogoro uliopelekea baina yangu na Menejimenti iliyokuwa ikisimamia ngoma ya Sherehe kushindwa kuelewana, ikumbukwe iliachia ngoma ya Sherehe sambamba na ngoma ya Baba la Baba lakini sijafanyia video”.

Hata hivyo Baba Levo amesema mwaka huu anatarajia kuachia ngoma si chini ya 20 akianza na ngoma ya Yes! No! aliyomshirikisha Ney Wamitego na kupikwa na Mr T Touch “Mwaka huu nimepanga kuachia magoma tu, mwaka huu pekee yake natarajia kuachia ngoma 20 nina ngoma nyingi zinakaa tu ghetto mpaka zinabebana na ninauwezo wa kuachia ngoma kila weekend, mwendo ni ule ule kuna komaa kaa chini juu jivu”.

 
Top