Menu
 

Mwanamuziki Jebby aliyefanya vizuri kupitia ngoma za Swahiba, Kastori na nyinginezo amesema ataurudia mfumo wake wa zamani wa kuimba nyimbo zenye kuelimisha ili kuwa tofauti na wasanii wengine ambao wamejikita katika ujumbe wa mapenzi.
''Mimi nadhani ni style ambayo kwanza ilinitambulisha kwenye muziki ni style ambayo watanzania walinipokea kwa moyo mmoja kwa hiyo ndio ulikuwa msingi wangu ndio maana nikawa Jebby kwa hiyo siwezi kuuacha na inaniuma navyofanya tofauti na hivyo'' Msanii Jebby alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Redio Bomba FM Mbeya.

Kwa hatua nyingine Jebby amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kupokea mfululizo wa nyimbo zake zenye uhalisia na ujumbe wa kuelimisha ''Mashabiki wangu nawaahidi na nawaambia nitafanya ngoma na watashangaa kwa sababu na uzoefu wa nhyimbo kama hizo nafikiri nitakata kiu ambayo walikuwa nayo kwa muda mrefu wa kupata ngoma zenye maudhi hayo''.
 
Top