Menu
 


Na Ezekiel Kamanga
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Itezi Mashariki Lameck Talian Kalendu na Mtendaji wa Mtaa Mariam Ngole wanatuhumiwa kufuja fedha za Mtaa zaidi  ya shilingi milioni nne zilizopatikana kutokana na mauzo ya viwanja vya ujenzi wa ujenzi wa vibanda vya biashara.

Ttuhuma hizo zimetolewa mbele ya mkutano wa hadhara uliosimamiwa na Diwani wa Kata ya Nsalaga Timoth Mandondo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na Mwenyekiti wa Mtaa Aman Kapinga.

Wakioneshwa kitendo cha ukosefu wa uadilifu wa viongozi hao baada ya kupokea taarifa ya mwenyeki wa mtaa baada ya viongozi hao kukiri kupokea shilingi milioni nne laki nane na elfu ishirini lakini walikataa kutia sani taarifa waliyoiandaa wenyewe.

Hali hiyo ilpelekea Halmashauri ya mtaa kuitisha mkutano ili wananchi waamue mustakabali wa suala hilo ambapo halmashauri ilikosa maamuzi hivyo kuomba ridhaa ya wananchi waamue hatua za kuchukua.

Baada ya Mvutano mkubwa wananchi kwa pamoja walimtaka Mwenyekiti Kapinga kumtaka Diwani Mandondo amuombe mkurugenzi kumchukulia harua za kinidhamu ili fedha hizo zirejeshwe kwa wananchi.

Fedha hizo zilitokana na uuzwaji wa viwanja 125 lakini taarifa yao ilionesha ni viwanja 97 tu ndivyo vilivyouzwa na kusababisha hasara kwa mtaa huo bila kutoa stakabadhi kwa fedha zilizopokelewa na mkutano kutoa siku tano fedha ziwe zimerejeshwa vinginevyo watawaburuza mahakamani.
 
Top