Menu
 

Jamii imetakiwa kuwa makini na matumizi ya mitandao ili kuepusha hatari ya kupata hatia na kifungo kupitia sheria mpya ya mtandao.

Wito huo umetolewa na mmoja wa wanasheria wa Serikali mkoani Mbeya Eunice Masigata katika semina ya kupitia sheria ya mtandao ambayo imeandaliwa na wizara ya mawasiliano na sayansi na teknolojia.

Amesema kupitia sheria hiyo watu watakaobainika kutumia mitandao vibaya watachukuliwa hatua za kisheria. 

Naye Mkuu wa upelelezi wilaya ya Momba ambaye amewakilisha jeshi la polisi mkoa wa mbeya Mtaki Kurujira amesema makosa ya mtandao yapo kidunia ambapo awali jeshi la polisi lilikuwa halina uwezo wa kufuatilia kesi hizo kutokana na kukosa nguvu kisheria.
 
Top