Menu
 

Na Ezekiel Kamanga,Dar es Salaam.

Mwananaharakati wa kupinga ukatili wa Kijinsia Pofesa Amina Mama kutoka Nigeria amewataka wananchi nchini kilinda amani na utulivu uliopo nchini ili kuepusha vurugu licha ya vuguvugu la kisasa lililopo nchini kwa sasa.

Profesa Amina ameyasema hayo katika Tamasha la Mtandao wa Jinsia nchini(TGNP) mwaka 2015 linalofanyika Makao Makuu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki mia nne kutoka mikoa mbalimbali nchini .

Mwanaharakati huyo amesema demokrasia ikivunjika huleta vitendo vya ukatili na mapigano kama ilivyotokea nchini Nigeria ambapo wasichana zaidi ya 300 wametekwa na magaidi hivyo kukatishwa masomo yao na kufanywa wake zao kitendo kichovunja haki za binadamu.

Aidha ametaka wanawake wasiwe nyuma kuwapigia kura wanawake waliojitokeza ili kuleta mabadiliko ambapo wanawake wengi ndiyo wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali kama elimu,afya na maji.

Hata hivyo katika Tamasha hilo wakufunzi mbalimbali walitoa mada katika makundi na baadhi ya makundi yameaaswa kuwa makini katika kazi zao na kutimiza majukumu yao wakiwemo Waandishi wa Habari ambapo Melkizedeki Karol amesema Waandishi wanapaswa kuyaelewa mambo mengi na kuwaelimisha wananchi.

Karol amesema vyombo vya habari vinapaswa kutoa nafasi sawa kwa utoaji habari hasa katika kipindi cha  kampeni za uchaguzi ambapo utafiti unaonesha wanaume wamepewa aslimia 79 na wanawake asilimia 21 tu hali inayoonesha hakuna usawa katika vyombo vya habar licha kuwa wanawake ni zaidi ya aslimia 53 ya wananchi wote nchini.
 
Top