Menu
 

Ongezeko la watu nchini limetanjwa kuchangia ukosefu wa dawa na vifaa tiba kwenye baadhi ya vituo vya afya hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi, mama na mtoto jiji la Mbeya Nginael Ngowo ambapo amesema tatizo hilo pia limekuwa likichangiwa na mwitikio mdogo wa jamii kutumia huduma za uzazi wa mpango.

Aidha amesema kati ya wanawake 110,499 jijini Mbeya wanawake wanaotumia njia za uzazi wa mpango 41,989 sawa na asilimia 38.

Asilimia 38 Ya wanawake wa jiji la Mbeya ndio wanaotumia njia ya uzazi wa mpango ya muda mfupi na kwamba wanaotumia njia ya muda mrefu ni asilimia 23.

Hata hivyo Ngowo amesema mwitikio wa wanaume katika huduma za afya ya uzazi ni mdogo kutokana na kutokuwa na elimu sahihi ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
 
Top