Menu
 

Hitmaker wa Walawala, Urudi na Coconut CHRIS BEE ametangaza kuachia ngoma yake mpya siku za usoni inayokuja na video yake, ngoma hiyo iitwayo BASHEE inakuwa ni ngoma yake ya Nne katika orodha ya ngoma alizoziachia.

Akipepeta maneno kupitia kurasa zake zilizopo katika mitandao wa kijamii kama ku-share taarifa na mashabiki wake ameandika hivi.. " Haya usipitwe...... BASHEE ni ngoma mpya ambayo inaachiwa na VIDEO yake muda si mrefu(Wiki Ijayo), ni ngoma iliyopo katika miondoko ya AFRO POP na inachezeka....

BASHEE ina maana ya NI VIPI/NIAJE katika ngoma hii nimemshirikisha dada yangu aitwae PETRONIA (Petronia Yahya Mfaume) ambaye ana kipaji cha hali ya juu. Producer aliyeipika anaitwa KONA kutoka Bante Beatz na Mwongozaji wa Video anaitwa NICKLASS kutoka kampuni ya Imagenation.

Mdau wa muziki naomba usipitwe na jiandae kufanya updates ya playlist yako mara baada ya kuachiwa.

Naitwa CHRIS BEE Hitmaker wa ngoma za Walawala, Coconut na Urudi. Follow me on instagram @chrisbeeofficial
@chrisbeeofficial
@chrisbeeofficial "

BOFYA HAPA KUONA KIONJO CHA VIDEO YA NGOMA HIYO YA BASHEE.
 
Top