Menu
 

Meneja wa Diamond, Babu Tale akishirikiana Kalapina wamemchukua Chidi Benz na mkupeleka Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Babu Tale, Chidi Benz na Kalapina
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni rapa huyo kuomba msaada baada ya kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimkabili.
Kupitia instagram, Babutale amepost video na kuandika:
Mwana amekubari kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini
Katika video hiyo Babu Tale alisema wamefika salama Life and Hope Rehabilitation Organization, Huku Kalapina akiomba mungu kumsaidia Chidi Benz. 
 
Source:- BONGO 5
 
Top